*Ni baada ya nati za gari lake kung'olewa*
Na Mwandishi Wetu,
Mwanga-Kilimanjaro.
KATIKA kile kinachodaiwa ni vita ya kutafuta ubunge katika Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro, leo watu wasiojulikana wameng'oa nati za mbele za gari ya mgombea ubunge Shaibu Mruma.
Tukio hilo limetokea leo Julai 31.2025 akiwa katika Kata ya Mgagao ambapo wagombea wa ubunge kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani hapo wameanza kampeni ya kuomba kura kwa wajumbe wa chama hicho, kabla ya Agosti 4 kupigiwa kura.
Mruma amesema anahisi gari yake imefunguliwa nati za mbele walipokuwa wanajitambulisha na kujinadi kwa wajumbe.
"Tukio hilo limetokea limetokea leo tulipokuwa tumetokea kata ya Mgagao kuelekea kata ya Kiria ambapo baada ya kuona mtikisiko (webling) kwenye gari katika steling na mlio ilibidi nisimamishe gari kukagua ndio tulipogundua kwamba nati zote za matairi ya mbele zimefinguliwa," amesema.
Hata hivyo Mruma amesema hakuna madhara yeyote kwa mgombea wala mtu mwingine yeyote kutokana na kadhia hiyo.
Hakuna maoni: