Dar es Salaam, Septemba 26, 2025
Katika kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana nchini, Kampuni ya Gulf Jobs Hunts Manpower imezindua rasmi ofisi yake ya kwanza nchini Tanzania, ikiwa na dhamira ya kupeleka Watanzania zaidi ya 10,000 kufanya kazi katika nchi mbalimbali za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ikiwemo Dubai, Abu Dhabi, Sharjah, Ajman, Alain, Ras Al Khaimah na Fujairah.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Gulf Jobs Hunts Group, Mohamed Kashif amesema kampuni hiyo inalenga kutoa fursa za ajira kwa vijana wa Kitanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo ulinzi, usafi, udereva magari makubwa na madogo, pamoja na usaidizi wa mizigo viwanja vya ndege.Kwa upande wake, Meneja wa Gulf Jobs Hunts Manpower Tanzania, Bi Shamim Mohamed, ametangaza nafasi 5,000 za ajira kwa madereva wa teksi katika UAE, ambapo usaili utafanyika katika ofisi za kampuni hiyo kuanzia Oktoba 6 hadi 7 mwaka huu.
Bi Shamim alieleza kuwa madereva watakaochaguliwa watapatiwa manufaa kadhaa yakiwemo:
➡️ Visa ya ajira ya miaka miwili
➡️ Leseni ya udereva ya UAE
➡️ Nyumba ya kuishi
➡️ Usafiri wa kazini
➡️ Bima ya afya
➡️ Likizo moja kwa mwaka
Kwa upande wake, mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Bi Zainab Suleiman, ameipongeza kampuni hiyo kwa kuanza kutoa huduma zake nchini na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutatua changamoto za ajira hususan kwa vijana.Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu Kikosi cha Mbwa na Farasi, Afande Hamis Siojo, pamoja na Diwani wa Kata ya Chang’ombe, Mheshimiwa Kelvin Mhinde Mhlidze, ambao kwa pamoja walisisitiza umuhimu wa kampuni hiyo kuzingatia sheria na haki za wafanyakazi watakaoajiriwa.
Ofisi za Gulf Job Hunts zipo Keko jijini Dar es salaam kituo cha mabasi cha bora, karibu kabisa na sheli na sheli ya oil link.

Hakuna maoni: