SERIKALI YA CCM YAWEZESHA UPANUZI WA KIWANDA CHA SARUJI MAWENI TANGA KUONGEZA UZALISHAJI NA AJIRA


Upanuzi wa Kiwanda cha Chokaa na Saruji cha Maweni Limestone Limited (Huaxin Cement Co. Ltd.)

Chini ya uongozi wa Rais Samia Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji. Kuboreshwa kwa mazingira hayo kumewezesha upanuzi wa mradi wa kiwanda cha Maweni Limestone Limited ambacho kinazalisha saruji aina ya Huaxin kilichopo katika Jiji la Tanga. 

Awali kiwanda hicho kilikuwa hakizalishi malighafi muhimu katika uzalishaji wa saruji inayoitwa ‘clinker’, baada ya upanuzi kiwanda kimefanikiwa kuzalisha ‘clinker’ kwa ajili ya uzalishaji wa saruji kwa matumizi yake na matumizi ya viwanda vingine. Aidha upanuzi wa mradi huo umegharimu dola za Marekani milioni 30 na umeajiri jumla ya watu 906 ambapo wazawa ni 424, wageni 82 na wenye mikataba kutoka kwa mzabuni ni 400. 

Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha clinker tani milioni 1.24 kwa mwaka na saruji tani milioni 1.5 kwa mwaka. Chini ya uongozi wa Rais Samia imani ya uwekezaji imeongezeka kwa wawekezaji kutokana na mazingira mazuri yaliyowekwa na serikali.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.