SERIKALI YA DKT SAMIA YAANZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAGADI SODA ENGARUKA KUCHOCHEA VIWANDA NA KUPUNGUZA UAGIZAJI NJE
Chini ya uongozi wa Rais Samia, Serikali imeanza kutekeleza mradi Magadi Soda ambao utaimarisha upatikanaji wa malighafi mbalimbali za viwandani.
Mradi huu kwa muda mrefu umekuwa katika mikakati mbalimbali ya Serikali ambapo hapo awali utekelezaji wake ulielekeza katika eneo la Ziwa Natroni lakini kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo za kimazingira ulikwama. Juhudi za serikali ya awamu ya sita zimepelekea kupatikana kwa eneo la Engaruka wilaya ya Monduli mkoani Arusha ambapo hatua za utekelezaji zimeanza ikiwemo kufanya tathmini ya eneo hilo na kulipa fidia kisha kutafuta wazabuni na kufanya uwekezaji. Hadi sasa Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 5.8 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi wa eneo hilo ambapo hadi kufikia Aprili, 2025 jumla ya shilingi bilioni 5.7 zimelipwa kwa wafidiwa 528 kati ya wafidiwa 595 sawa na asilimia 88 ya wafidiwa wote. Zoezi la ulipaji fidia linaendelea kwa wafidiwa 67 waliobaki.
Mradi huu pia umetangazwa ili kupata wazabuni watakaoutekeleza na utekelezaji wake utasaidia upatikanaji wa malighafi muhimu za viwanda hapa nchini hivyo kupunguza uagizaji wa malighafi hizo nje ya nchi.

Hakuna maoni: