SERIKALI YA RAIS DKT. SAMIA YAWEKEZA ZAIDI YA BILIONI 32 KUBORESHA SOKO KUU LA KARIAKOO



Chini ya uongozi wa Rais Samia, Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam limepangwa kufanyiwa maboresho makubwa ili kuimarisha biashara za jumla na rejareja katika jiji la kibiashara la Tanzania. Soko hili lina historia ndefu tangu enzi za ukoloni, na kwa sasa linahudumia maelfu ya wafanyabiashara na wateja kila siku. Soko hili linakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya USD milioni 13, sawa na shilingi bilioni 32, kwa mujibu wa bajeti iliyotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la kisasa.

Linatarajiwa kuhudumia watu 5,500 kwa siku, sawa na watu 2,007,500 kwa mwaka. Linajumla ya vizimba 2,000 na linaweza kuhifadhi magari 600 kwa mpigo. Soko hili ni kielelezo cha ukuaji wa uchumi wa miji mikuu na biashara za kitaifa chini ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Litaajiri jumla ya wajasiriamali 4,500, ambapo ajira rasmi zitakuwa 2,000 na ajira zisizo rasmi ni 2,500, hakika Tanzania ni njema atakaye na aje.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.