KANGA-SONGWE
Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mheshimiwa Fadhili Nkurlu, amezindua vifaa vya kutambua na kudhibiti moto katika Shule ya Sekondari Kanga, hatua inayolenga kuimarisha usalama shuleni, hasa kwa shule za bweni.
Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi, walimu na wanafunzi, DC Nkurlu alisema hatua hiyo ni muhimu kupunguza athari za moto kwenye taasisi za elimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, CPA Cecilia Kavishe, aliahidi kuendelea kusambaza vifaa hivyo kwenye shule nyingine za bweni wilayani humo.
Mkuu wa shule, Ester Ole Kimani, alisema walimu na wanafunzi wamepewa mafunzo ya kutumia vifaa hivyo pamoja na mbinu za kujikinga dhidi ya moto, huku wanafunzi wakionyesha uelewa wao kupitia maonesho ya vitendo.
Jamii imepongeza jitihada hizi, ikihimiza usambazaji wa teknolojia hiyo kwa shule zote nchini.

Hakuna maoni: