MRADI WA MAJI SAME–MWANGA–KOROGWE KUBORESHA HUDUMA KWA WANANCHI 300,000


Mradi wa Maji wa Same–Mwanga–Korogwe Sh. Bil 406.07.

Chini ya Rais Samia, Mradi wa Same–Mwanga–Korogwe unagharimu Shilingi Bilioni 406.07 (takribani USD milioni 156) na unatekelezwa katika Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga kwa manufaa ya wananchi 300,000. Mradi huu utazalisha maji lita milioni 51.65 kwa siku, sawa na lita bilioni 18.85 kwa mwaka. Kukamilika kwa mradi huu kutaleta mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa maji kwa wananchi, na serikali inalenga kufikia asilimia 95 ya upatikanaji wa maji mijini na asilimia 85 vijijini ifikapo mwaka 2030.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.