Mradi wa Maji wa Morogoro wa Shilingi Bilioni 185.
Chini ya Rais Samia, Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) inatekeleza mradi wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 185 katika Manispaa ya Morogoro, kwa ufadhili kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).
Mradi huu unalenga kuboresha Bwawa la Mindu na miundombinu ya maji, ikiwemo ujenzi wa mtambo mpya wa kutibu maji eneo la Mafiga, na utaongeza uzalishaji wa maji hadi lita milioni 89 kwa siku, ukilinganisha na mahitaji ya lita milioni 86 kwa mwaka 2025.
Mradi utahudumia wakazi wa mitaa ya Kasanga na Mgaza, ambapo idadi ya wananchi imeongezeka kutoka 3,918 mwaka 2014 hadi 10,000 kwa sasa.

Hakuna maoni: