Biharamulo.
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Balozi Simon Sirro amesema ameendelea kukoshwa na kazi zinazofanywa na STAMICO) huku akiahidi serikali inaendelea kuwekeza katika mgodi wa STAMIGOLD
Balozi Sirro ametoa kauli hiyo alipotembelea na kukagua maendeleo ya mgodi wa STAMIGOLD uliopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera na kisha kuzungumza na Menejimenti na watumishi wa mgodi huo unao milikiwa na kusimamiwa na STAMICO.
Amesema Bodi imejipanga kusimamia kikamilifu mgodi huo kupitia Menejimenti ya STAMICO ili kuendelea kuongeza uzalishaji na kuleta tija zaidi.
Amekiri STAMIGOLD tangu ianze 2013 imepiga hatua kubwa kwa kujitegemea kwa maana ya kuendesha shughuli zak ikiwemo manunuzi bila kutegemea hazina.
Aidha Sirro ameiagiza STAMIGOLD kuendelea kujikita kwenye tafiti ili kubaini maeneo yanayofaa kwa uchimbaji na kuweza kupanua uwigo wa uwekezaji na kufikia malengo ya kuongeza mapato.
Sirro ametumia nafasi hiyo pia kusisitiza nidhamu katika matumizi ya fedha za umma kwa watendaji walioaminiwa na kupewa nafasi mbalimbali za kusimamia na kuendesha mgodi huo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Deusdedith Magala amesema STAMIGOLD tayari imeanza miradi mipya kwenye maeneo matatu ya uchimbaji yanayotarajiwa kuongeza uzalishaji.
“Kwa miezi minne ijayo, hadi kufikia Juni 2026 tunatarajia kuzalisha wakia za dhahabu 8,000, tunaamini kwamba kupitia hii itasaidia mgodi wetu wa STAMIGOLD kupiga hatua kubwa za kiuchumi”, amesema.
Amesema pia STAMIGOLD imejipanga kufanya tafiti kwenye leseni ambazo hazijawahi kuguswa ili kuongeza uhai wa mgodi huo kutoka miaka mitano ijayo na kufikia zaidi ya miaka 10.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa STAMIGOLD, Ali Said amesema mpaka sasa mgodi umajiri wafanyakazi 613 ambao wanapambana kutimiza wajibu wao ili kuongeza mapato ya mgodi.
Amesema tangu mwaka 2013, STAMIGOLD imechangia kiasi cha sh bilioni 56 serikalini na juhudi zinaendelea kuhakikisha uwekezaji uliofanyika unasaidia watanzania kupata manufaa ya mgodi.
Ali ameihakikishia Bodi ya Wakurugenzi ya STAMICO kuwa utatuzi wa changamoto zilizopo utachochea kiwango cha uzalishaji kutoka wastani wa kilo 30 dhahabu kwa mwezi.







Hakuna maoni: