Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi amewasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali, leo tarehe 27 Februari 2026.
Katika ziara hiyo, Waziri Ndejembi ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zinazoshughulikia na kusimamia shughuli za mafuta na gesi nchini.
Akiwa mkoani humo, Waziri Ndejembi atakagua na kuzindua miradi mbalimbali ya gesi asilia, ikiwemo uzinduzi wa zoezi la uchimbaji wa visima kuongeza uzalishaji wa gesi asilia pamoja na visima vya utafiti kwa ajili ya kuongeza hifadhi ya gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay na Ntorya.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa kuongeza matumizi ya gesi asilia kwa kuongeza upatikanaji wa gesi kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, matumizi ya viwandani na majumbani.





Hakuna maoni: