WITO umetolewa kwa wanafunzi hasa wa kike kusoma kwa bidi ili waweze kufikia malengo yao na kulisaidia Taifa kupata wataalamu wazuri hapo baadae.
Rai hiyo imetolewa leo Mapema jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Rasilimari watu kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB),Suzana Kiweru,wakati wakitoa msaada wa Taulo za Kike kwa wanafunzi wa Temeke Sekondari ikiwa ni kuelekea kwenye sherehe ya siku ya wanawake Duniani.
"Ninawaomba niwatie moyo wanafunzi wa kike wanaopata hedhi,wasikate tamaa kwasabu hii maana ni hali ya Kimaumbile,mnatakiwa mjikite kwa kusoma kwa bidii mfikie malengo yenu"Amesema Suzana.
Hata hivyo,Suzana ametumia nafasi hiyo kuwasihi wanafunzi wa kiume kutojihusisha kwa jambo lolote litakalopelekea kukwamisha jitihada za mtoto wa kike kwenye kukosa elimu ikiwemo masuala ya mapenzi.
"Tunaomba wasichana na wakiume sote mshirikiane katika masomo yetu ili tuweze kufikia malengo yetu""Amesema.
Kwa Upande wake Mchumi kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB),Neema Mkemwa.amewataka wanafunzia kuvumilia changamoto wanazokutana nazo kwa kusoma kwa bidii wakati serikali ikitatua changamoto wanazokumbana nazo.
"Someni kwa bidii hapa shuleni,changamoto zipo,na serikali yenu inafanya jitihada kubwa za kutatua,bodi ya mikopo tupo sekta ya elimu kuhakikisha mnafikia malengo ya kwenda chuo kikuu"Amesema Neema.
Aidha,Neema ,amesema kuelekea siku ya wanawake Duniani amewataka wanafunzi hao kutambua hali za kijinsia ni za wanawake na wanaume kwa kuwatia moyo wanawake mbalimbali ikiwemo michango yao mbalimbali kwenye jamii.
Naye Mkuu wa Shule ya Temeke Sekondari,Ingi Mtenga,ameishukuru HELSB kwa hatua yao ya kuwasaidia taulo za kike wanafunzi hao na kusema itakuwa chachu kwao kufanya vizuri.
Pia naye mwanafunzi Temeke Sekondari,Joice James,ameishukuru bodi hiyo kwa msaada huo wa Taulo za kike.


Hakuna maoni: