JOWUTA YAPATA NAFASI CORI, KUIMARISHA SAUTI ZA WANAHABARI

 


Na Mwandishi Wetu. 

CHAMA cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), kimepitishwa rasmi kuwa mwanachama wa Taasisi ya Wadau Wanaopigania Haki za kupata Habari (CoRI).

JOWUTA wamepitishwa na CoRI katika kikao chake cha tatu kilichofanyika Desemba 5 mwaka jana, baada ya chama hicho kutuma maombi ya kujiunga kutokana na jukumu lake kubwa la kutetea na kulinda maslahi na uhuru wa wafanyakazi katika vyombo vya habari Tanzania.

Mwenyekiti wa CoRI, Ernest Sungura amesema wanachama wa taasisi hiyo wametambua mchango mkubwa wa JOWUTA kupigania haki za waandishi wa habari, kuhamasisha usimamizi wa sheria ya habari, kujengea uwezo wa kitaaluma na kupigania uhuru na maadili ya uandishi, jambo ambalo linaendana na dhumuni la CoRI.

"Tunawakaribisha CoRI tushirikiane kupigania sekta ya habari ili iweze kusonga mbele zaidi kwa pamoja,"amesema.

Mwenyekiti wa JOWUTA, Mussa Juma amesema uamuzi wa CoRI kupokelewa kuwa mwanachama una faida kubwa kwa JOWUTA ambayo ina wanachama zaidi ya 400 nchi nzima.

Juma amesema JOWUTA itatoa ushirikiano wa dhati kuhakikisha sekta ya habari inaendelea kukuwa zaidi.

"JOWUTA tunaamini hatua hii ni kubwa kwetu kwani hivi karibuni tulitangazwa pia kuwa wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) na tunaamini kuwa mwanachama kwenye taasisi hizi tutaongeza sauti za wanahabari kudai hali bora kazini,kuthaminiwa lakini pia kufanya kazi Kwa Uhuru"amesema

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.