KAMPUNI YA H&J YAINGIA KWENYE MGOGORO WA ARDHI



Na Mwandishi Wetu.

KAMPUNI ya H &J Limited imeshtakiwa katika Baraza la Ardhi la Kata ya Bwilingu kwa tuhuma za kuingia kimakosa katika shamba ukubwa wa hekari moja na nusu maeneo ya Magome ndani ya Halmashauri ya Chalinze.

Meneja Msaidizi wa Kampuni hiyo, Haji Abdallah alidai walinunua hekari 13 na nusu na walifuata taratibu zote za manunuzi.

"Tulinunua Februari mwaka 2026, tulilipa fedha na ofisi ya Mwenyekiti Magome inafahamu mikataba ya mauziano,"alidai Haji.

Mwenyekiti wa Magome, Iddi Royal alipoulizwa kuhusu mgogoro huo alidai tayari ulishafikishwa Baraza la Ardhi la Kata hawezi kuzungumzia.

Kampuni hiyo inadaiwa kuchukua hekari moja na nusu za shamba jirani linalosimamiwa na Salumu Rajabu maarufu Mzee Mpole na kusababisha eneo hilo lililokuwa hekari nne kupungua na kubakia hekari 2 na nusu 

Kwa mujibu wa hati ya manunuzi ya shamba hilo hilo la hekari nne inaonyesha lilinunuliwa Machi mosi mwaka 2018.

"Shamba tulinunua kwa Degwa Honga hekari 4 kwa Sh 1,600,000 na nilikuwa shahidi, shahidi wa aliyeuza alikuwa anaitwa Adamu Tegule,"alidai Mzee Mpole.

Alisema eneo limeharibiwa kuanzia juu kushuka chini na Kampuni hiyo ilifanya hivyo kwa ajili ya kutengenezea mfereji juu unaounganisha sehemu ya chini yenye chanzo cha maji waweze kutengeneza mabwawa ya maji.

"Kinachohitajika ni eneo lililichukuliwa waliachie, Mwenyekiti kashindwa kutupa ushirikiano hata tulipomfata kwa ajili ya kupata ufafanuzi sababu ofisi yake inamtambua aliyavamia eneo hilo alikataa kutusaidia,"alisema.

Alisema baada ya kukosa ushirikiano waliamua kwenda Baraza la Ardhi la Kata kufungua malalamiko ambapo pande mbili ziliitwa na baraza hilo lilimwamuru Haji kuita mashahidi Machi 23 mwaka huu na siku hiyo Baraza litafika eneo la tukio 

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.