WMA - DODOMA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Alban Kihulla amewaelekeza wajumbe wa
menejimenti ya Wakala hiyo kuwa na majadiliano ya wazi na yenye tija yanayolenga kuboresha zaidi huduma kwa wananchi hivyo kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kujenga nchi.
Ametoa wito huo mapema leo Machi 26, 2026 wakati akifungua kikao kazi cha Menejimenti kilichoketi kupitia utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka 2025/26 na kupitia mpango na bajeti wa mwaka wa fedha 2026/27.
"Majadiliano yetu yawe ya wazi na kila mmoja atoe mchango wenye tija kwa manufaa ya Taifa letu," amesisitiza.
Aidha, Mtendaji Mkuu Kihulla amewataka wajumbe wa kikao hicho kinachofanyika katika ukumbi wake wa Makao Makuu, eneo la Medeli Dodoma, kuhakikisha wanaudadavua na kuuchambua kwa kina mpango na bajeti ya mwaka wa fedha ujao ili kuwezesha utekelezaji wenye tija.
Wakala wa Vipimo iko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara na ina jukumu kuu la kumlinda mlaji kupitia uhakiki na usimamizi wa matumizi sahihi ya vipimo.








Hakuna maoni: