RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MATENKI 15 YA KUHIFADHI MAFUTA DAR


DAR ES SALAAM. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa matenki 15 ya kuhifadhi mafuta huku akiahidi Serikali itaendelea kuimarisha ushirikishwaji wa sekta binafsi ili kuongeza ufanisi kwenye huduma za bandari kwani tokea kuingia kwa mwekezaji Dp World imesaidia kuboresha huduma za bandari kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza machi 3,2026 Jijini Dar es salaam katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwenye ujenzi wa tenki za kuhifadhia mafuta kwenye bandari ya Dar es Salaam Rais Dkt. Samia ameagiza ujenzi huo kukamilika kwa wakati na kwa ubora pia amesema ujenzi huo uwe chachu ya kuimarika kwa upatikanaji wa huduma za mafuta nchini

Aidha katika kuimarisha ushirikishwaji na sekta binafsi Rais Dokta Samia ameagiza kuongeza uwazi na mifumo kusomana kwa mamlaka za bandari TPA na Mamlaka ya Mapato TRA ili kuhakikisha ujenzi huo unaleta tija na kuepuka upotevu wa mapato kwani lengo ni kuimarisha uchumi wa nchi

Kwa upande wa Waziri wa Uchukuzi Professa Makame Mbarawa amesema kukamilika kwa ujenzi huo itaongeza uwezo wa mamlaka ya bandari kutoa huduma za bandari kwa mataifa mbalimbali ya Afrika kwenye sekta ya mafuta huku akisisitiza kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi pamoja na kuimarisha shughuli za bandari

Akitoa Taarifa fupi ya mradi huo wa ujenzi wa matenki ya kuhifadhia mafuta,Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya bandari Plasduce Mbossa amesema mradi huo wenye matenki 15 ya kuhifadhi na kusambaza mafuta unajengwa na wakandarasi kutoka china kwa gharama ya shilingi bilioni 678.6 na unatarajia kukamilika mwaka 2027.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amesema uwepo wa maghala ya Serikali ya kuhifadhia mafuta ni muhimu katika kulihakikishia Taifa kuwa na hifadhi ya mafuta ambapo amesema Jiji hilo lima maghala 22 ya kuhifadhia mafuta yanayomilikiwa na watu binafsi

Vilevile RC Chalamila amemshukuru na kumpongeza Rais Dokta Samia kwa namna anavyotoa fedha kuboresha miundombinu ya bandari na barabara ambapo amesema kuongezeka kwa foleni jijini humo kunatokana na kazi nzuri inayofanywa na bandari huku akisisitiza kuwa kwa sasa wanaandaa mwarobaini wa changamoto hiyo ya foleni.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.