Soko la Hisa la Dar-es-Salaam (DSE) limesema kwa mwezi wa pili mwaka huu thamani ya mtaji imefikia Trilioni 34.6 katika makampuni 28 ambayo yameorozeshwa .
Huku Makampuni ya 22 ya ndani ambayo yameorezeshwa thamani ya mtaji imefikia trilioni 24.2.
Hayo yamebainishwa mapema leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Bw. Peter Nalitolela,wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitoa taarifa ya soko kwa mwezi wa pili.
Amesema ni ongezeko kubwa ukilinganisha mwezi wa pili mwaka jana ambapo thamani ya mtaji ilikuwa Trilioni 19 huku kwa mwaka jana mwezi wa pili thamani ya mtaji kwa makampuni ya ndani ilikuwa Trilioni 12.1.
"Tukilinganisha mwaka hadi mwaka kwa asilimia soko letu limekuwa likikuwa kwa kasi kubwa,tunawashukuru wawekezaji"amesema .
Hata hivyo,Nalitolela,amesema kuhusu mifuko ya pesheni ya watumishi wa umma na sekta binafsi ambayo imewekeza kwenye soko la hisa thamani imeongezeka kwa asilimia 80.8.
Pia Mtendaji mkuu huyo,amegusia kuhusu mifuko ya uwekezaji na kusema imeongezeka kwenye soko ilo huku pia kwa mwezi wa pili mwaka huu thamani ya miamala imefikia bilioni 242 zimepita kwenye soko hilo ikilinganisha na Bilioni 34.8 kwa mwezi wa pili mwaka jana.
"Ongezeko hili ni ishara ya wawekezaji wameendelea kuliamini soko,na wawekezaji wamezidi kuwekeza na kununa hisa ndio imepelekea thamani miamala kuongezeka"ameongeza
Kadhalika ,Nalitolela,amesema katika kipindi cha mwezi wa pili mwaka huu Akaunti zilizounganishwa DSE kiganjani zimefikia 193545 ukilinganisha mwaka jana mwezi wa pili akaunti zilikuwa 58123 ni ongezeko la asilimia kubwa.
Aidha,Nalitolela,amewapongeza mawakala wa soko la hisa ,wafanyakazi kwa kuchangia soko hilo kukua siku hadi siku,na kutumia nafasi hiyo kuwataka watanzania kujiunga na DSE kiganjani kupata taari mbalimbali.

Hakuna maoni: