Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Ilala Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) Salum Morimori amewataka wamiliki wa magari yanayosafirisha wanafunzi kuajili madereva wenye sifa ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza kutokana na madereva hao kutotokidhi vigezo.
Morimori ameyasema hayo leo March 16, 2026 katika viwanja vya shule ya Msingi Olimpio wakati wa ukaguzi wa magari ya kusafirisha wanafunzi uliofanywa na Jeshi la Polisi kuhakikisha vyombo hivyo vinakidhi vigezo vya kusafirisha wanafunzi.
"Kabla hujamwajiri dereva wako hakikisha anakidhi matakwa ya kisheria. Hakikisha ana leseni hai angalau daraja C1 au C, awe amesoma, weka kumbukumbu zake, fanya ukaguzi wa gari lako dereva asije kukudanganya kwani gari hilo likipata shida na wewe mmiliki tutakuuliza" amesema Morimori
Aidha amewataka madereva wa magari hayo kukagua magari yao kabla ya kuingia kazini na kuwataka kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Naye mwakilishi wa Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Ilala Mrakibu mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) Sarah Bundala amewataka madereva kuweka maudhui yenye kuwajenga watoto kimaadili na kuacha kuweka maudhui yasiyofaa kama vile nyimbo zinazohamashisha ngono.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati ya shule ya Upanga Bwana Abel Kasabalala amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kukubali mwaliko wao, ambapo amesema aliwaomba kuja kufanya ukaguzi wa magari hayo ili kujua ubora na ubovu na wao kama wamiliki wachukue hatua






Hakuna maoni: