BORA KUZUI UHALIFU KABLA HAUJATOKEA KULIKO KUPAMBANa NA UHALIFU

Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Sospeter Mkama amewaasa wenyeviti wa serikali za mitaa kuwapa ushirikiano Polisi kata ili kutengeneza muunganiko mazuri baina ya wananchi na Jeshi la Polisi.

Kamishna Mkama ameyasema hayo April 01, 2026 katika viwanja vya Polisi wilaya ya Chanika Mkoa wa Ilala wakati akizungumza na wenyeviti wa Serikali za mitaa wilaya ya Kipolisi Chanika katika ziara yake Mkoa ni humo.

Ameongeza kuwa ni bora kuzuia uhalifu kuliko kupambana na uhalifu, hivyo amewaasa wenyeviti kutoa ushirikiano kwa Polisi ili kufikia dira ya Polisi ya kuwa na jamii yenye kiwango kidogo cha uhalifu na utii wa sheria.

"Ni bora kuzuia uhalifu kuliko kusubiri utokee, hivyo elimu itakayotolewa na Polisi kata itasaidia kuzuia uhalifu kabla haujatokea" Amesema CP Mkama.

Baadhi ya wenyeviti wa Serikali Mtaa wamepongeza juhudi za Jeshi la Polisi na wamesema kwa sasa changamoto yao kubwa ni migogoro ya ardhi ambapo wameeleza kuwa kuna wimbi la watu wananzisha miradi ya maendeleo pasipo kuwashirikisha wamiliki wa maeneo kitu ambacho kinapekelekea migogoro.

Aidha wameomba kuharakishwa kwa ujenzi wa vituo vya Polisi, Kata ya Buyuni na Msongola ili kusogeza huduma ya Polisi kwa wananchi.

Katika hatua nyingine CP Mkama.amezungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa wilaya ya Chanika na kuwaelekeza mambo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Polisi. 

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.