SPIKA AAGIZA WAZIRI NA KAMATI YA BUNGE KUJADILI MWENENDO WA MAFUTA NCHINI



DODOMA

Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Zungu, amemuagiza Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kujadili mwenendo wa mafuta nchini, ikiwemo gharama zake pamoja na uhakika wa upatikanaji wake.

Ametoa maelekezo hayo leo tarehe 01 Aprili, 2026, Bungeni Jijini Dodoma, akieleza kuwa kukosekana kwa mafuta kunaweza kusababisha kukwama kwa utekelezaji wa mipango mbalimbali ya nchi pamoja na shughuli nyingine muhimu.

Maelekezo hayo yanakuja kufuatia tangazo la Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) la bei elekezi mpya za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, zilizoanza kutumika rasmi kuanzia leo Aprili Mosi, 2026, ikiwa ni sehemu ya marekebisho yanayozingatia mwenendo wa soko la dunia.

Sababu kuu ya kupanda kwa bei hizo ni mgogoro unaoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, hususan kati ya Marekani, Israel na Iran, ulioanza Februari 28, 2026, na kuathiri kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mafuta duniani.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.