ENG. SAMAMBA, WATAALAMU WIZARA YA MADINI WAJADILI MPANGO MKAKATI WA KUKUZA, KUIMARISHA MCHANGO WA SEKTA
Dodoma
Wataalamu wa Wizara ya Madini wakiongozwa na Katibu Mkuu, Eng. Yahya Samamba, wamekutana kujadili mwelekeo wa mpango mkakati unaolenga kuongeza mchango wa Sekta ya Madini katika ukuaji wa uchumi wa taifa. Kikao hicho kilijikita katika kubaini maeneo yenye tija kubwa, ikiwemo uongezaji thamani wa madini, uwekezaji wa teknolojia, na uboreshaji wa mazingira ya uchimbaji na biashara ya madini.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Aprili 21, 2026, Jijini Dodoma, Eng. Samamba alisisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa rasilimali madini, akieleza kuwa mpango huo unapaswa kuendana na dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2050 kwa kuhakikisha sekta inakuwa shindani kimataifa na yenye manufaa kwa wananchi.
Menejimenti ya Wizara imeazimia kuimarisha uratibu kati ya taasisi za sekta, kuongeza ushirikishwaji wa sekta binafsi, na kuharakisha mageuzi ya kisera na kisheria ili kuwezesha ukuaji endelevu wa sekta ya madini nchini.








Hakuna maoni: