CAIRO.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba ameshiriki katika maadhimisho ya sherehe za Muungano zilizoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Misr, Jijini Cairo April 26, 2026.
Mhe. Salome amepata wasaa wa kukutana na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Misri Mej. Gen Richard Makanzo, Mwenyekiti wa Diaspora ya Watanzania waishio nchini Misri Bi. Zaituni Abdallah pamoja na watanzania wanasoma fani mbalimbali kutoka Chuo cha Alexandria.
Mhe. Salome yupo nchini Misri kushiriki Mkutano wa East African Power Pool (EAPP) ambao unakutanisha Nchi wanachama kwaajili ya kujadili masuala muhimu katika umoja huo ikiwepo miradi ya uunganishaji wa Gridi na biashara ya kuuziana Umeme baina ya Nchi wanachama.
Mkutano wa EPP unatarajiwa kuudhuriwa na Nchi wanachama 13 ambao ni Burundi, Congo DRC, Djibout, Misri ambaye ndiye mwenyeji wa mkutano huo, Ethiopia, Kenya, Libya, Rwanda, Somalia, Sudani Kusini, Sudani Kaskazini, Uganda na Tanzania.








Hakuna maoni: