MKURUGENZI TAA AWATAKA WATANZANIA KUPIGIA KURA UWANJA WA NDEGE WA NYERERE.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania TAA, Bw. Abdul Mombokaleo, amewataka Watanzania na wadau mbalimbali kupiga kura kwa wingi ili Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere JNIA kiweze kushinda tuzo ya “Africa’s Leading Airport 2026” kwenye World Travel Awards 2026.

JNIA imeteuliwa kuwania tuzo hiyo ikiwa pamoja na viwanja vya kimataifa vya Cape Town, Jomo Kenyatta na O.R Tambo. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa kampeni ya upigaji kura, Bw. Mombokaleo alisema kushinda tuzo hiyo kutaiweka Tanzania kwenye ramani ya ubora wa sekta ya usafiri wa anga kimataifa.

Naye Mkurugenzi wa JNIA, Bi. Bertha Bankwa, amewahakikishia Watanzania kuwa JNIA inastahili kushinda tuzo hiyo kwa sababu ya ubora wa huduma zake, si kwa sababu tu ya kura. 

JNIA ilishinda tuzo sawa hiyo mwaka 2025 kama "Kiwanja Bora Barani Afrika" kutoka World Travel Awards. Watanzania wanaweza kupiga kura kupitia barcode au kiungo kilichopo kwenye taarifa rasmi za TAA.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.