NCHIMBI : MALKIA WA NGUVU TUMIENI MAJUKWAA YENU KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewataka waandaaji wa tamasha la Malkia wa Nguvu kutumia majukwaa yao kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini ili kuwafikia wanawake wengi zaidi na kuchochea mabadiliko chanya katika matumizi ya nishati safi nchini.

Hayo ameyasema hayo wakati wa Kilele cha Tuzo kwa Wanawake waliofanya vizuri katika Sekta mbalimbali maarufu kama Malkia wa Nguvu jijini Dodoma ameeleza kuwa ili kuboresha mazingira na ustawi wa wananchi wanawake wana nguvu kubwa ya kupunguza madhara yatokanayo nanmatumizi ya nishati isiyofaa (kuni na mkaa) ambayo yamekuwa yakisababisha uharibifu wa mazingira na magonjwa ya mfumo wa upumuaji.

Amesema kuwa takribani asilimia 99 ya shughuli za upishi majumbani hufanywa na wanawake, hivyo wanayo nafasi kubwa ya kuwa chachu ya mabadiliko kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia

 Aidha, amepongeza juhudi za taasisi ya Clouds Media kwa kuandaa matamasha ya Malkia wa Nguvu ambayo yamekuwa yakilenga kumuinua mwanamke wa Kitanzania kijamii na kiuchumi huku akiongeza kuwa Serikali imejipanga kuboresha mazingira ya upatikanaji wa nishati safi ya kupikia ili kuboresha afya za Watanzania.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.