MAKONGORO NYERERE, LODHIA WAIBUKA WASHINDI WA WORLD CUP CANADA KUPITIA TEMBO CARD 🔥



Na Mwandishi Wetu,

Dar es Salaam. 

Kampeni ya “Fainali Ndo Mpango” kupitia Tembo Card Visa ya CRDB Bank imeendelea kutengeneza gumzo nchini baada ya droo ya pili kuibua majina makubwa, wakiwemo viongozi na wafanyabiashara maarufu waliofanikiwa kujishindia safari ya kwenda kushuhudia fainali za FIFA World Cup 2026 nchini Canada.

Miongoni mwa walioibuka washindi ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere, ambaye pia ni mtoto wa Baba wa Taifa hayati Julius Nyerere. Makongoro ameonekana kuwa mmoja wa majina yaliyovuta hisia kubwa katika droo hiyo iliyochezeshwa leo. 

Mbali na Makongoro, mshindi mwingine aliyeibua gumzo ni Arun Vithaldas Lodhia, anayehusishwa na familia ya wawekezaji wakubwa wa viwanda nchini kupitia Lodhia Industries, kampuni inayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa za chuma na plastiki Tanzania. 

Katika droo hiyo, washindi watatu wamejinyakulia safari ya kwenda Canada kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia 2026. Washindi hao ni Abdulrauf Suleiman Muta wa Dar es Salaam, Charles Makongoro Nyerere wa Sumbawanga pamoja na Arun Vithaldas Lodhia.

Sambamba na hilo, washindi wengine watatu wamejishindia TV janja za kisasa za inchi 85. Waliofanikiwa kushinda ni Amina Kaswala Awadhi wa Dar es Salaam, Esther Dauson Kabakama pamoja na Lusekelo Michael Mwamwala wa Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo, CRDB Bank pia ilikabidhi rasmi TV kwa washindi waliopatikana katika droo iliyopita, huku ikiendelea kuwahamasisha Watanzania kutumia Tembo Card Visa katika miamala yao ya kila siku ili kuongeza nafasi za kujishindia zawadi mbalimbali.

Viongozi wa kampeni hiyo wamesema droo na zawadi bado zinaendelea, huku wakitangaza kuwa kuanzia mwezi ujao kutakuwa na droo kubwa zaidi yenye zawadi nono kwa wateja wa benki hiyo.

Kampeni ya “Fainali Ndo Mpango” imeendelea kuvutia maelfu ya Watanzania kutokana na kutoa nafasi ya kipekee ya kushuhudia moja kwa moja michuano ya FIFA World Cup 2026 pamoja na kujishindia zawadi za kisasa kupitia matumizi ya Tembo Card Visa. 

Katika hafla hiyo ya droo ya pili ya kampeni ya “Fainali Ndo Mpango”, shughuli ya kuchezesha droo iliongozwa na Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kadi kutoka CRDB Bank, Karington Chahe, akishirikiana na Esther kutoka CRDB pamoja na balozi na influencer wa benki hiyo, Queens Masanya, ambapo waliongoza zoezi hilo lililowapata washindi wa safari ya kwenda Canada kushuhudia FIFA World Cup 2026 pamoja na washindi wa TV janja za inchi 85.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.