MBETO AIPA HEKO SMZ KUPANDISHA MISHAHARA YA KIMA CHA CHINI

Na Mwandishi wetu, 

Zanzibar.

Chama Cha Mapinduzi kimeipongeza kwa dhati SMZ chini ya Rais wake Dk Hussein Ali Mwinyi kwa kupandisha mshahara kima cha chini kutoka laki 3 hadi laki 5.

CCM kimeitaka SMZ kuendelea mkakati wa kutazama hali za maslahi ya Wafanyakazi wa kima hicho ili waweze kustawisha na kujijenga kiuchumi 

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar ,Idara ya itikadi ,Uenezi na Mafunzo, Khamis mbeto Khamis mara baada ya smz kutangaza kima kipya cha mshahara visiwani humu

Mbeto alisema ongezeko hilo la mshahara kwa kima cha chini ni fursa nyingine kwa Wafanyakazi kitakachosaidia katika kustawisha maisha yao.

Alisema kupanda mshahara huo mpya bila shaka smz imezingatia hali ya uchumi na maisha ya kila mzanzibari, garama za maisha na kuwapa motisha wafanyakazi,wazidi kusimamia majukumu yao kwa ufanisi.

'Siku zote motisha huongeza tija kazini. Tunawahimiza Wafanyakazi wote katika taasisi za umma, Wizara ,Idara na sekta zote wakasimamie nidhamu ya kazi ili kuongeza kasi ya uzalishaji "Alisema Mbeto 

Aidha,alisifu uongozi wa SMZ Awamu ya Nane kwa kujali na kutazama na kuinua hali za wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji ahadi za kisera na ahadi binafsi za Rais.

"Tokea aingie madarakani Rais Dk Mwinyi hii ni mara ya pili kupandisha mshara kima cha chini. Anafanya haya yote kwa kujali watu na maisha yao.Ungwana wa mtu ni kutenda si kusema maneno matupu"Alieleza Mbeto 

Hata hivyo , Mwenezi huyo alisema CCM kitaendelea kuzishauri mara kwa mara serikali zake ili zihakikishe maisha ya wananchi yanakimbizana na hali halisi ya kiuchumi.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.