RC CHALAMHLA AWASIHI VIJANA KUHUSU MACHAFUKO



DAR ES SALAAM. 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka vijana wasiharibu maisha yao kwa siasa na propaganda za chuki, badala yake wajikite katika jitihada kwa kuwa ndio siri pekee ya mafanikio katika maisha yao.

Amesisitiza maisha si mepesi kama wengi wanavyodhani, ni magumu na hayako kwenye propaganda ya vinywa na maneno mengi, bali lazima upitie magumu ili ufanikiwe.

Chalamila ameeleza hayo leo Mei 16, 2026 alipozungumza katika Kongamano la Vijana wa Vyuo Vikuu lililobeba ujumbe wa 'Never Again'.

"Pamoja na kupata elimu mnayoipata leo, mchawi wa kweli ni kujimudu kimaisha na namna pekee ya kujimudu kimaisha ni kuyatafsiri maisha kwa namna ya kipekee," amesema.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.