Tabora
Serikali imeiwezesha Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupata dola milioni 65 kwa ajili ya utekelezaji wa matengenezo ya miundombinu ya barabara kupitia mfuko wa dharura (CERC).
Mhandisi Seff amesema fedha hizo ni mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia uliotolewa kufuatia tathmini ya uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua za El-Nino za mwaka 2024.
Amesema tathmini hiyo ilibaini maeneo mengi ya barabara yaliyoharibiwa na hivyo kuhitaji matengenezo ya haraka ili kurejesha mawasiliano na huduma kwa wananchi.
“Miradi hii inatekelezwa nchi nzima na kwa wastani utekelezaji wake umefikia asilimia 70. Kazi zote zinatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 2026,” Alisema.
Aidha, amesema miradi hiyo inatekelezwa na makandarasi wazawa huku akiwasisitiza Mameneja na wasimamizi wa TARURA nchini kuongeza usimamizi ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa viwango vinavyotakiwa.
Akizungumzia ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Seff amesema ameridhishwa na ubora wa kazi inayoendelea na kusisitiza kuwa miundombinu inayojengwa inapaswa kudumu na kupitika wakati wote ili kuwawezesha wananchi kufikia masoko, shule na kusafirisha pembejeo za kilimo.
Pia aliwataka wananchi kuitunza miundombinu inayojengwa kwa kuwa Serikali kupitia TARURA inaendelea kuwekeza fedha nyingi kuboresha miundombinu nchini.







Hakuna maoni: