Dar es Salaam.
Mchezaji wa timu ya kikapu ya Dar City na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Hasheem Thabeet amemkabidhi jezi maalumu gwiji wa soka wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand katika tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda.
Awali, wachezaji wa Dar City walikutana na kupata chakula cha pamoja na Ferdinand ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano ya michezo kati ya Tanzania na Uingereza.
Tukio hilo limeelezwa kuwa mwanzo wa ushirikiano mpana wenye lengo la kuendeleza mchezo wa kikapu nchini, kuvutia uwekezaji katika sekta ya michezo pamoja na kuunganisha wadau wa michezo wa Tanzania na Uingereza.
Katika mazungumzo yao, Thabeet na Ferdinand walijadili mikakati ya kukuza vipaji vya vijana kupitia programu shirikishi, kuimarisha miundombinu ya mafunzo pamoja na matumizi ya teknolojia katika maendeleo ya wanamichezo.
Viongozi hao pia walisisitiza umuhimu wa kuwa na mifumo endelevu ya mafunzo, kliniki za michezo na programu za kubadilishana uzoefu wa kimataifa ili kuwapa vijana nafasi zaidi ndani na nje ya nchi.








Hakuna maoni: