Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kupitia mradi wa ECOFISH unaofadhiliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Denmark kupitia DANIDA, inaendelea kutoa elimu ya matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwa wavuvi na wakulima wa mwani katika maeneo ya pwani ili kuboresha shughuli zao za kiuchumi na usalama wao.
Kupitia semina na ziara za wataalamu wa TMA, wananchi wamepatiwa uelewa wa namna ya kutumia taarifa za hali ya hewa katika kupanga shughuli za uvuvi na kilimo cha mwani, huku mradi huo pia ukiwezesha tafiti na ufadhili wa masomo kwa wataalamu wa sekta ya uvuvi na hali ya hewa.
Msimamizi wa mradi huo, Dkt. Sarah Emerald Osima, amesema ECOFISH inalenga kuimarisha huduma za tahadhari za mapema na kuongeza ustahimilivu wa jamii dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi. Wananchi wa Wilaya ya Wete wamepongeza elimu hiyo wakisema imewasaidia kuelewa umuhimu wa kufuatilia taarifa za hali ya hewa kabla ya kwenda baharini.

Hakuna maoni: