DAR ES SALAAM
Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) kinatarajia kuwakutanisha mawakili, wanamichezo na wadau mbalimbali Oktoba 31 mwaka huu katika Jiji la Dodoma kupitia mbio maalum za Wakili Marathon zitakazolenga kuchagiza utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi.
Akizungumza kuhusu maandalizi ya marathon hiyo, Mwenyekiti wa TPBA, Addo November amesema tukio hilo pia linalenga kuhamasisha afya, michezo na mshikamano katika jamii.
Amesema Watu mbalimbali mashughuli wataudhulia katika Marathon hiyo Akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari, Msanii Faridi kubanda maarufu kama Fid Q pamoja na mwanariadha nguli Alphonce Simbu ambao wanatarajiwa kushiriki katika mbio hizo.
Kwa mujibu wa waandaaji, viingilio kwa washiriki vitaanzia Shilingi 40,000 hadi 100,000 kulingana na aina ya ushiriki, huku watoto nao wakitengewa Fun Marathon maalum pamoja na vifaa vya kushiriki mbio hizo.
“Pamoja na kuwa wataalamu wa sheria na kutetea watu mahakamani, hata kwenye mbio pia tupo. Mimi binafsi nimejisajili kukimbia kilomita 21,” amesema Addo November.
“Mchezo wa marathon ni mchezo mama, karibu kila mchezo unahusisha kukimbia kwa namna moja au nyingine,” amesema Ikangaa.







Hakuna maoni: