WAZIRI WA NISHATI, MHE. DEOGRATIUS NDEJEMBI AKUTANA NA BALOZI WA NORWAY KUIMARISHA USHIRIKIANO WA SEKTA YA NISHATI

Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Tone Tinnes, kwa lengo la kuimarisha na kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Norway katika sekta ya nishati.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Mei 22, 2026 katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ikiwemo ushirikiano wa kimkakati katika maendeleo ya gesi asilia, umeme, nishati jadidifu pamoja na kubadilishana uzoefu wa kitaalamu kwa ajili ya kukuza sekta hiyo katika nchi hizo mbili.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kamishna wa Mafuta na Gesi kutoka Wizara ya Nishati, Goodluck Shirima, pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo na Uzalishaji kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Paschal Njiko na wataalamu wengine kutoka sekta ya nishati.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.