Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam.
Benki ya CRDB imehitimisha rasmi kampeni yake ya “Fainali Ndo Mpango na TemboCard Visa” baada ya kuandaliwa kwa kipindi cha miezi mitatu, ambapo jumla ya washindi 20 wameibuka na kujipatia zawadi mbalimbali zenye thamani kubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 11, 2026, Meneja Mwandamizi wa Kadi wa CRDB, Karington Chahe, alisema kampeni hiyo ilianza Februari 12, 2026 na imehitimishwa leo kwa mafanikio makubwa.
Kwa mujibu wake, washindi 10 watapata nafasi ya kipekee ya kuhudhuria mashindano ya Kombe la Dunia, ambapo sita watafikia nchini Canada na wanne nchini Marekani, safari zote zikigharamiwa na benki.
Aidha, washindi wengine 10 wamepata televisheni za kisasa za inchi 85 pamoja na ving’amuzi kama sehemu ya zawadi za kampeni hiyo.
Chahe alieleza kuwa kampeni hiyo imepokelewa vyema na wateja wa benki, hali iliyochochea ongezeko la matumizi ya TemboCard Visa katika miamala mbalimbali ya kidijitali.
Aliongeza kuwa CRDB itaendelea kuboresha huduma zake na kuanzisha kampeni zaidi zitakazowahamasisha wateja kutumia mifumo ya kisasa ya malipo huku wakinufaika na zawadi mbalimbali.

Hakuna maoni: