GEOFREY KILIBA AENDELEA KUONYESHA UONGOZI WA VITENDO KWA WANAFUNZI

MAKALA.

Tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Wasomi, Geofrey Kiliba ameendelea kuonyesha dhamira ya dhati ya kusimamia na kutetea maslahi ya wanafunzi kupitia uongozi unaozingatia ukaribu, usikivu na utatuzi wa changamoto zinazowakabili wanafunzi katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu.

Ndani ya kipindi kifupi tangu aingie madarakani, Kiliba amefanya ziara katika vyuo mbalimbali nchini, hatua inayotafsiriwa na wengi kuwa ishara ya kujali na kuthamini maoni ya wanafunzi anaowaongoza. Kupitia ziara hizo, amekuwa akikutana na wanafunzi moja kwa moja, kusikiliza changamoto zao na kujadiliana nao kuhusu namna bora ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na ustawi wao kwa ujumla.

Wakati wa kampeni na baada ya kupewa dhamana ya uongozi, Kiliba aliahidi kuwa sauti ya wanafunzi na mlinzi wa maslahi yao. Ahadi hiyo inaonekana kutekelezwa kwa vitendo kupitia juhudi zake za kufika maeneo mbalimbali na kujionea hali halisi ya maisha na mahitaji ya wanafunzi.

Miongoni mwa vyuo alivyovitembelea hadi sasa ni Chuo cha Maji, Chuo cha Ustawi wa Jamii, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), MSJ, Jordan University pamoja na Chuo Kikuu cha Ardhi na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).

Uongozi bora hupimwa kwa matendo, uwajibikaji na uwezo wa kusikiliza wanaowaongoza. Kwa mtazamo huo, hatua zinazochukuliwa na Rais wa Wasomi Geofrey Kiliba zinaendelea kujenga imani miongoni mwa wanafunzi na kuonyesha nia ya dhati ya kuimarisha ustawi wao pamoja na mazingira ya elimu.

Wanafunzi na wadau mbalimbali wa elimu wanaendelea kumuunga mkono katika juhudi zake za kuendeleza maslahi ya wanafunzi na kujenga msingi imara wa maendeleo katika sekta ya elimu ya juu nchini.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.