Na Francisco Peter,
Dar es Salaam
Neno "wanandinga" ni msamiati wa michezo unaomaanisha wachezaji wa mpira wa miguu (kandanda).
Neno hili hutumika sana katika lugha ya mitaani na vyombo vya habari vya michezo nchini Tanzania kumaanisha watu wanaoonesha uwezo wa kucheza mpira.
Sasa hapa linamuibua kinyozi anaye wapendezesha nyota kibao tu kwa kuwanyoa stahili nyingi .
Stanley James ambaye ndiye mmiliki wa STANBLENDS HAIR STUDIO iliyopo kwenye jengo la Salamander mtaa wa Samora Avenue (Near Askari Monument)
Anasema yopo maeneo ya mjengo akinyoa mitindo tofauti tofauti ambao kwa kuwa eneo lipo katika maeneo nyeti kabisa ya mdhamini mkubwa wa klabu maarufu ya jangwani pita pita za wanandinga na watu maarufu mitaa ya Posta Jijini Dar es Salaam wamekuwa wakifika kufuata huduma bora.
Ikumbukwe kuwa Tajiri wa klabu ya Yanga Gharib Said Mohammed (GSM) ,mwenye mkwanja wa maana akiifanya yanga kuwa na matarajio mema ya kujitwalia ubingwa wa Tanzania bara na kuingia mara kwa mara kwenye michuano ya Kimataifa.
Ndiye mwenye mjengo wa Salamander na ni hali ya kawaida wanandinga kupisha pishana katika mjengo huo wa Salamander.
Stanley akiwa ndiye kinyozi na mmiliki wa biashara ya kutoa huduma bora ya salon anasema; namekuwa na viwango vizuri katika kunyoa mitindo yote .
"Tumekuwa tukizingatia ubora anaotaka mteja , ninaovimnyozi wengine wafuatao takribani sita ambapo wanajituma kufanya kazi kama sehemu ya kujipatia kipato ," anasema kinyozi huyo.
Anaeleza kuwa kazi ya kutoa huduma hii kwa sasa ni itaji kwa wanadamu imekuwa ni sehemu ya vijana wenzake kujipatia kipato hivyo vijana wa Sasa wasichague kazi .
Anabainisha mafanikio kwa nyakati hizi ni kuhamua ufanye kazi na uokote mishiko mambo ya maokoto yanaleta maendeleo katika kutimiza malengo mbali mbali.
Kuhusiana na KOMBE la Dunia 2026 likiwa limeanza kwa takwimu zinazothibitisha kwa mara nyingine kuwa soka ndio mchezo wenye mvuto mkubwa zaidi duniani .
Stanley anaeleza kuwa ni matazamio mengine ya kuiga mitindo ya mastaa, huko kwenye kombe la dunia wateja upendelea staili mpya zinazoibuka hivyo kuja kutaka mitindo watakavyo kwa kuwa wateja wao wanaofika Salon upendelea aina mbali mbali ya mitindo.


Hakuna maoni: