Katika hatua inayoonyesha kuongezeka kwa mchango wa wataalamu wa Kitanzania katika majukwaa ya Kimataifa kampeni ya Perterms Consultancy Limited imetangazwa mshindi wa mchango wa Share My Story Initiative ulioandaliwa na Taasisi ya Basel Institute On Governance kupitia Mkutano wa Kimataifa wa Sita wa Hatua za Pamoja (Collective Action).
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo Mtendaji Mkuu wa Perterms Shakibu Nsekela amesema mpango huo ulilenga kutoa jukwaa Kwa wataalamu na Taasisi mbalimbali Duniani kubadilisha uzoefu kuhusu namna ya ushirikiano wa wadau unavyoweza kuimarisha uwajibikaji, usimamizi, wa hatari na uadilifu katika biashara Taasisi.
Aidha Nsekela amesema kuwa ushindi huo wa Perterms umeelezwa Kuwa si tu mafanikio kwa kampuni hiyo bali ni ishara ya kuongezeka kwa mchango wa Tanzania katika mijadala ya Kimataifa kuhusu utawala bora na ujenzi wa mifumo imara ya Taasisi na biashara.
Perterms Consultancy Limited ni Kampuni ya Kitanzania ya ushauri iliyobobea katika utawala bora, usimamizi wa hatari, uzingatiaji wa Sheria na kanuni, Uchunguzi wa Udanganyifu, Uadilifu, Uangalizi wa kina wa Taasisi na Miradi Pamoja na urejeshaji wa mali.
Sambamba na Hilo Kampuni hiyo husaidia taasisi za umma na Sekta binafsi kuimarisha uwajibikaji, kudhibiti hatari na kuboresha utendaji kupitia suluhisho za kitaalamu zinazotegemea ushahidi wa kiutafiti na uzoefu.
Mtendaji Mkuu Nsekela alimaliza Kwa kusema Kuwa Perterms imejijengea uzoefu kupitia ushirikiano na Taasisi za sekta binafsi, mashirika ya maendeleo na uwekezaji katika kuimarisha mifumo ya utawala, kuongeza uwazi katika maamuzi ya biashara na kuimarisha uwezo wa Taasisi kutanbua na kudhibiti hatari kabla hazijaleta madhara makubwa.


Hakuna maoni: