"TALII NA SABASABA" MAKUMBUSHO YA TAIFA LA TANZANIA YAWAKARIBISHA WANANCHI KATIKA MAONESHO YA 49 YA KIMATAIFA YA BIASHARA (SABASABA) 2026
Makumbusho ya Taifa la Tanzania yanawakaribisha wananchi wote kutembelea banda lake katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) 2026, yaliyoanza rasmi leo, tarehe 28 Juni 2026, katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
Katika banda la Makumbusho ya Taifa, wageni watapata fursa ya kujionea kijiji cha utamaduni kinachoakisi maisha halisi ya Kitanzania, kujifunza historia na urithi wa Taifa, pamoja na kufurahia vyakula vya asili, sanaa, mila na desturi mbalimbali zinazotambulisha utajiri wa tamaduni za Tanzania.
Wananchi na wageni wote wanahimizwa kutembelea banda la Makumbusho ya Taifa ili kujifunza, kuburudika na kuthamini urithi wa Taifa letu.
"Talii na Sabasaba 2026 – Tujifunze, Tuthamini na Turithishe Urithi Wetu"








Hakuna maoni: