TARURA YATOA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA SABASABA 2026 ‎

 


‎Dar es Salaam.

‎Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia banda la Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kutoa elimu na huduma mbalimbali kwa wananchi wanaotembelea Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

‎Maonesho hayo yaliyoanza rasmi tarehe 28 Juni 2026 yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 13 Julai 2026 huku ufunguzi rasmi ukitarajiwa kufanyika tarehe 3 Julai 2026.

‎Wataalamu wa TARURA wanatoa elimu ya ana kwa ana kuhusu majukumu ya wakala, miradi ya maendeleo ya barabara za vijijini na mijini pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi.

‎Aidha, wananchi wanapata fursa ya kuuliza maswali, kutoa maoni na mapendekezo pamoja na kupatiwa ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na TARURA na taasisi nyingine zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.