WAZIRI KOMBO AKUTANA NA RAIS WA KOICA JIJINI SEOUL

SEOUL 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo amefanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA), Bw. Chang Won-sam, katika mkutano uliofanyika Juni 1, 2026 jijini Seoul. 

Mkutano huo ulijikita katika kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na KOICA, hususan katika sekta za elimu, afya, teknolojia ya habari na mawasiliano, pamoja na ujenzi wa uwezo wa rasilimali watu. 

Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Waziri Kombo alishukuru mchango unaotolewa na  KOICA katika kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuimarisha uwezo wa taasisi za umma. 

Alisema,  ushirikiano baina ya Tanzania na  Jamhuri ya Korea   umeendelea kukua na kuimarika  sikunhata siku kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini humo mwaka 2024, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana na KOICA ili kufukia Malengo ya maendeleo endelevu. 

Kwa upande wake, Rais wa KOICA, Bw. Chang Won-sam,  alisisitiza dhamira ya shirika hilo kuendelea kushirikiana kwa karibu na serikali katika kutekeleza miradi yenye matokeo chanya kwa maslahi mapana. Alibainisha kuwa KOICA itaendelea kuunga mkono mipango inayochochea ubunifu, maendeleo ya teknolojia na ukuaji jumuishi wa uchumi. 

Rais huyo pia alitumia fursa hiyo, kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake katika kukuza uchumi wa nchi kupitia kuimarisha ushirikiano na nchi mbalimbali na Mashariki ya kikanda na kimataifa. 

Mhe. Waziri Kombo yupo nchini Korea kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Korea na Afrika unaotarajiwa kuhitimishwa tarehe 2 Juni, 2026.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.