Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Mbeya limetoa amri ya kusimamisha kwa muda usiojulikana usikilizaji wa Maombi Madogo Na. 12 ya Mwaka 2026, yaliyofunguliwa na Fidel Alphonce Ntanyinya dhidi ya Frank Nicholaus Chawe, likisubiri uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu maombi ya mapitio yaliyowasilishwa na upande wa mjibu maombi.
Katika uamuzi huo, Baraza limeamuru kuwa Frank Nicholaus Chawe na mtu yeyote anayehusiana naye hawaruhusiwi kuingia, kutumia au kuuza eneo la ardhi linalobishaniwa hadi shauri la msingi litakapomalizika.
Wakati huo huo, Fidel Alphonce Ntanyinya ameruhusiwa kuingia katika eneo hilo na kuweka walinzi kwa ajili ya kulinda mali zilizopo.
Aidha, Highland Auction Mart imeagizwa kutekeleza amri hiyo, huku Kamanda wa Polisi wa Mji Mdogo wa Mbalizi (OCD) akitakiwa kusimamia utekelezaji na kuhakikisha usalama wakati wa zoezi hilo.
Amri hiyo imesainiwa tarehe 15 Julai 2026, na taarifa ya utekelezaji imeelekezwa kuwasilishwa tarehe 22 Julai 2026.
#DhahabuOnlineTV #Mbeya #Ardhi #Mahakama #Habari

Hakuna maoni: