KAIMU MENEJA MKUU TGDC ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA NISHATI SABASABA

Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mha. Shakiru Idrissa Kajugus, ametembelea banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Mha. Kajugus amepata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara ya Nishati kwa wananchi wanaotembelea banda hilo.

Wizara ya Nishati inaendelea kutoa elimu na huduma mbalimbali kuhusu sekta ya nishati, ikiwemo umeme, gesi asilia, nishati safi ya kupikia na maendeleo ya miradi ya kimkakati, katika banda lake lililo karibu na banda la TANESCO.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.