NAIBU WAZIRI SALOME AWASILI MOROGORO KUFUNGUA WARSHA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Mussa Kilakala, akiwasili katika Ukumbi wa Morena Hotel mkoani Morogoro kwa ajili ya kufungua warsha ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari pamoja na Maafisa Mawasiliano wa Serikali kuhusu uandishi na uhamasishaji wa masuala ya Nishati Safi ya Kupikia.

Warsha hiyo imeandaliwa na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), kupitia Mradi wa CookFund unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Salome ameambatana na Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia wa Wizara ya Nishati, Bw. Nolasco Mlay, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Nishati, Bi. Nteghenjwa Hosseah na Meneja wa Mradi wa CookFund – UNCDF, Bw. Imanuel Muro.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.