Na Mwandishi Wetu
WAKULIMA nchini wameshauri kutumia mbolea hai zilizothibitishwa na Mamlaka ya Kudhibiti Mbolea Tanzania (TFRA), ikiwemo Mc Donald Volca Grow, ili kuleta tija kwenye kilimo.
Ushauri huo umetolewa leo Julai 3, 2026 jijini Dar es Salaam na Ofisa Utetezi na Ushawishi wa Kilimo Hai kutoka Taasisi Mwavuli ya Kuendeleza Kilimo Hai Tanzania (TOAM), Paul Chilewa, ambapo amesema mbolea hizo zina matokea chanya kwenye kilimo.
Chilewa ameitolea mfano Mbolea Mc Donald Volca Grow ambayo ni kirutubisho cha asili kilichotengenezwa kutokana na aina tano za mawe ya miamba ambayo yana virutubisho vya udongo na kuuhuisha na kurudi kwenye asili yake.
Ofisa huyo alitaja sifa nyingine ya mbolea hiyo ni kujaza mizizi ya mimea na kuufanya kuwa na nguvu, kuwepo vikonyo vingi na kupelekea maua na matunda kuwa mengi kutokana na virutubisho kama Zinc na Boron.
Amesema pia mbolea hiyo inafukuza wadudu kwenye mmea kutokana na salfa iliyopo na kupunguza magonjwa kama vile fangasi.
"Mc Donald Volca Grow ni mbolea bora kwani inawekwa mara moja shambani kwa kipindi cha miaka mitatu hadi minne," amesema.
Chilewa ametaja vitu vilivyotengeza mbole hiyo ni Nitrojeni, Phosphorus, Potassium, Calcium Magnesium, Carbonate (CaMg (Co3)2) na Trace Minerals.
Amesema mbolea ya Mc Donald Volca Grow ni kirutubisho bora na chenye matokeo bora kwa mkulima.






Hakuna maoni: