WIZARA YA NISHATI YAENDELEA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI KATIKA BANDA LAKE SABASABA

Wizara ya Nishati na taasisi zake inaendelea kuwahudumia wananchi wanaotembelea banda lake katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Leo, Julai 3, 2026, ni siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho hayo yanayoadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1976.

Maonesho hayo yanafunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Daniel Chapo akiwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika maonesho hayo, Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na taasisi zake inaendelea kutoa elimu na huduma mbalimbali kuhusu sekta ya nishati, ikiwemo umeme, gesi asilia, mafuta, nishati safi ya kupikia na nishati jadidifu.

Wananchi wanaotembelea banda la nishati pia wanapata fursa ya kufahamu mafanikio ya Serikali, miradi inayoendelea kutekelezwa pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi zilizo chini ya Wizara.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.