Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Ellen Maduhu amemuaga Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Mhe. Christine Grau, baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini.
Bi. Maduhu amempongeza Balozi Grau kwa mchango wake katika kuimarisha ushirikiano wa uwili kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa kimkakati kwa ajili ya maendeleo endelevu na ustawi wa wananchi wa pande zote mbili.
Kwa upande wake, Balozi Grau ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano alioupata wakati wa kipindi chake cha uwakilishi nchini na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya katika nyanja mbalimbali za maendeleo.



Hakuna maoni: