KIKWETE APOKEA UGENI WA VIONGOZI KUTOKA SOMALIA WALIOKUJA TANZANIA KUJIFUNZA UTENDAJI WA SERIKALI NA MIFUMO YA UTUMISHI WA UMMA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete wiki hii Alhamisi Agosti 28, 2026 kwenye Ofisi ya Wizara iliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma ameongoza mapokezi ya ujumbe wa Serikali ya Somalia ukiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Utumishi Ndg. Hirsi J. Ganni uliokuja nchini kwa ajili ya kujifunza utendaji wa Serikali na mifumo ususani mabadiliko makubwa ya kimifumo ya utumishi wa umma yaliyofikiwa Tanzania.
"Ujio wao wenzetu wa Somalia ni kuja kujifunza jinsi tumeboreka katika maeneo ya utumishi wa umma nini tunafanya na panapotokea changamoto za watumishi tunachofanya kusaidia watumishi. Wamekuja kuona pia jinsi mifumo yetu ya utumishi wa umma inavyofanya kazi
"Ziara hii ni kielelezo kwamba vitu tunavyofanya kwenye utumishi wa umma vinatambulika na kuthaminika nje ya mipaka yetu na haya ni mafanikio makubwa sana ambayo Serikali ya Awamu ya 6 inajivunia na Sisi kama Serikali kwa niaba ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan tunaishukuru sana Serikali ya Somalia kwa kuitambua Tanzania kama ina mifumo mizuri ya utumishi wa umma na hii ni kielelezo kizuri cha mafanikio ya Serikali ya Rais Samia.
Ziara hii viongozi na wataalamu kutoka Somalia watapata nafasi pia ya kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu kujifunza mahusiano jinsi Serikali inahusiana na wananchi wake, jinsi Serikali inasimamia masuala ya ajira na kazi, usalama mahali pa kazi na pensheni ili kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili.



Hakuna maoni: