Na. WMA- Dodoma
Wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na wananchi wameendelea kutembelea banda la Wakala wa Vipimo (WMA) Katika siku ya tano ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea jijini Dodoma, wakipatiwa elimu kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi ya vipimo.
Katika maonesho hayo, wananchi wamekuwa wakipata fursa ya kujifunza namna ya kutumia na kuhakiki vifaa vya vipimo, pamoja na kuelewa madhara yanayotokana na matumizi ya vipimo visivyo sahihi katika biashara za mbegu, pembejeo, maziwa, mazao na bidhaa nyingine.
Wataalamu wa WMA wamekuwa wakitoa elimu kwa vitendo na kujibu maswali ya wananchi kuhusu taratibu za uhakiki wa vipimo, hatua inayolenga kulinda haki za wakulima, wafanyabiashara na walaji.
WMA imesema itaendelea kutoa elimu hiyo bure kwa wananchi katika siku zote za maonesho hayo, ikiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya vipimo sahihi kwa ajili ya kuongeza tija na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Kaulimbiu ya maonesho ya Nanenane Kitaifa 2026 ni: "Tambua Soko; Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050"





Hakuna maoni: