MAINSTREAM GROUP YAZINDUA MAIN PESA LOTTO KWA USHIRIKIANO NA ITHUBA

DAR ES SALAAM: 

Kampuni ya Mainstream Group, inayomiliki vituo vya habari vya Main FM na Main Digital nchini Tanzania, imeingia katika ushirikiano na Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa (iThuba) kuzindua mchezo mpya wa bahati nasibu unaojulikana kama Main Pesa Lotto.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mainstream Group, Deogratias Mosha, amesema Main Pesa Lotto inalenga kuwapa Watanzania fursa ya kushindania zawadi mbalimbali za fedha taslimu kupitia droo zinazofanyika kila baada ya saa tatu.

Mosha amesema mshiriki anaweza kushiriki katika droo tatu tofauti ambazo ni droo ya saa tatu, droo ya siku na droo ya wiki, kwa kutumia Shilingi 1,000 pekee.

Amesema kushiriki ni rahisi, ambapo mchezaji anatakiwa kutumia huduma za fedha kwa njia ya simu, ikiwemo M-Pesa, Tigo Pesa au Airtel Money, kuchagua sehemu ya Kulipia Bili, kisha kuingiza namba ya kampuni 711 777 na kumbukumbu ya malipo 123, kabla ya kufanya malipo ya Shilingi 1,000.

Mosha amesema mchezo huo uko wazi kwa Watanzania wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, huku matokeo ya droo yakitangazwa kupitia vituo vya redio, kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za Main Pesa Lotto pamoja na tovuti rasmi ya Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa iThuba Tanzania, Mark Wahome, amesema ushirikiano huo unalenga kusogeza huduma za bahati nasibu karibu zaidi na Watanzania kwa kutumia njia rahisi na nafuu zinazoweza kuwafikia wasikilizaji wa Main FM na wananchi kwa ujumla.

Wahome amesema ushirikiano huo pia unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za bahati nasibu kwa wananchi kupitia njia zinazowafikia kwa urahisi.

Viongozi wa Mainstream Group na iThuba wamewahimiza Watanzania wenye sifa kushiriki katika mchezo huo kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.