SEKTA BINAFSI YATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KUKUZA UCHUMI NA AJIRA

Mkurugenzi Mtendaji wa SF Group, Kelvin Koka, ametoa wito kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa za kiuchumi na uwekezaji ili kuchangia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 na kuongeza ajira kwa vijana.

Wito huo ameutoa Septemba 17, 2026, wakati akizungumza katika Kongamano la Kibiashara la 200 CEO Business Forum, akibainisha kuwa sekta binafsi ina nafasi kubwa katika kukuza uchumi.

Koka amesema lengo la sekta hiyo ni kuchangia asilimia 70 ya uchumi, hivyo wafanyabiashara wanapaswa kutumia fursa zilizopo na kuwekeza katika maeneo mbalimbali.

Amesema matumizi ya teknolojia, ikiwemo Akili Unde (AI), pamoja na kujenga mitandao ya kibiashara, yanaweza kuongeza ufanisi na ushindani wa kampuni katika biashara.

Akizungumzia ajira, Koka amesema ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kupitia sera wezeshi unaweza kusaidia kuanzishwa na kukua kwa kampuni nyingi, hatua ambayo itafungua fursa zaidi za ajira kwa vijana.

Amesema SF Group imejipanga kutumia maarifa yaliyopatikana katika kongamano hilo kuchukua hatua zitakazosaidia kuchangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.