Na Mwandishi Wetu.
Dodoma. Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-CENTRE), David Kafulila, amehudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Mji wa Serikali Mtumba, iliyofanyika leo, Oktoba 30, 2026, katika Viwanja vya Mashujaa, jijini Dodoma.
Hafla hiyo iliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan, imeweka alama muhimu katika juhudi za Serikali za kukusanya taasisi zake katika eneo moja kwa lengo la kuimarisha uratibu na ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi.
Ushiriki wa Kafulila katika hafla hiyo unaonesha umuhimu wa ushiriki wa taasisi za umma katika matukio ya kitaifa yanayolenga kuimarisha utendaji wa Serikali na kuchochea maendeleo ya nchi.





Hakuna maoni: