NIFFER JOVIN ASAINI MKATABA WA UBALOZI NA DERMA INTERNATIONAL

 Niffer Jovin asaini mkataba wa ubalozi na Derma International


DAR ES SALAAM. 

Uaminifu na ushawishi alionao katika mitandao ya kijamii ni miongoni mwa sababu zilizomfanya Niffer Jovin kuchaguliwa kuwa balozi wa Kampuni ya Derma International Limited, inayojihusisha na uuzaji wa samani na bidhaa mbalimbali za matumizi ya nyumbani na ofisini.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo Oktoba 13, Meneja wa kampuni hiyo, Hussein, alisema uamuzi wa kumchagua Niffer umetokana na utafiti alioufanya kupitia mitandao ya kijamii na kubaini kuwa ni miongoni mwa washawishi wanaoaminika na kupendwa na watu wengi.

Alisema baada ya kubaini sifa hizo, aliona anafaa kuwa mwakilishi wa kampuni hiyo katika kuitangaza na kuifikisha kwa wateja wengi zaidi, hivyo kuamua kuwasiliana naye kwa ajili ya kuanzisha ushirikiano huo.


Kwa upande wake, Niffer Jovin aliushukuru uongozi wa Derma International Limited kwa kumwamini na kumpa nafasi hiyo, akieleza kuwa amevutiwa na ukweli na uaminifu unaoonekana katika bidhaa za kampuni hiyo.

Alisema ameamua kushirikiana na kampuni hiyo kwa kuwa anaamini katika ubora wa bidhaa zake na hatapenda kuitangaza kwa wafuasi wake bidhaa ambayo haina uhalisia na sifa zinazotolewa.

Aaaaa

Niffer aliwahimiza wananchi kutembelea kampuni hiyo kupata mahitaji mbalimbali yakiwemo vitanda, viti, meza za kulia chakula, makapeti, mazulia na bidhaa nyingine za mapambo, huku akimpongeza Hussein kwa namna anavyohudumia wateja na kuwasaidia kuboresha mandhari ya nyumba zao.

Derma International Limited inatarajia kutumia ushirikiano huo kumfikia wateja wengi zaidi kupitia ushawishi wa Niffer katika mitandao ya kijamii.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.